Friday, September 9, 2016

SIMBA WAMRUHUSU LYANGA KUFANYA MAJARIBIO OMAN


Klabu ya Simba kupitia Ofisa Habari wake Haji Manara imethibitisha kuondoka kwa streika huyo wa wekundu wa msimbazi kuelekea Oman kwa majaribio na timu ya Oman Club kwa kufuata taratibu zote na kuruhusiwa na klabu yake.  

''Danny Lyanga amekwenda Muscat, Oman kwa ajili ya kufanya majaribio kwa muda wa wiki mbili kwenye klabu ya Oman Club na kama atafanikiwa sisi Simba hatuna tatizo katika kumwachia mchezaji kwenda kucheza soka la kulipwa''.    

Aliongezea kwa kusema ''Oman Club ni klabu kubwa kama Simba au Yanga kwa Tanzania, na kama atafanikiwa ni faida kwakwe, kwa klabu na taifa..'' Kwani ameondoka kwa kufuata taratibu zote za Simba.  

No comments:

Post a Comment