Tuesday, September 27, 2016
LEWANDOSKI AITAKA BAYERN IJIFUNZE KUTOKA KWENYE KIPIGO CHA ATLETICO.
Robert Lewandowski ameitaka Bayern Munich kujaribu aina tofauti ya kuikabili Atletico Madrid kesho Jumatano Septemba 28.
Lewandowski aliyaongea hayo baada ya msimu uliopita vijana wa Diego Simieno kupata ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali katika uwanja wa Vicente Calderon msimu uliopita, kabla ya 2-1 kwenye mechi ya marudiano ambayo Atletico waliingia fainali kwa bao la ugenini.
Lewandoski amekiri uwezo na uimara wa ulinzi wa Atletico lakini alisema inapaswa kuonyesha ilichojifunza kwa msimu uliopita kama watataka kuweza kushinda kwa mara pili kwenye kundi D.
''Siku zote wana ulinzi mzuri na wanaelewana,'' alisema mshambuliaji huyo, akiongea na vyombo vya habari kabla ya Bayern kupanda ndege kuelekea Madrid.
''Pale wanapofunga bao, wanajua kwamba watashinda mchezo kutokana na ulinzi wao.
''Tunahitaji kucheza tofauti kama mara ya mwisho tulivyocheza Madrid, na nina matumaini tutafanya vyema. Siku zote ni wapinzani wazuri na itatubidi kujaribu kufunga mabao.''
Thomas Muller ana uhakika wa kwamba wataweka viwango vya ushindi juu na kupunguza idadi ya makosa ili kuhakikisha ushindi wa tisa katika mechi tisa chini ya kocha wao mkuu Carol Ancelotti.
''Kwa yeyote anaejua soka anajua kwamba Atletico wanaruhusu mabao machache ,'' alisema mchezaji huyo wa taifa la Ujerumani.
''Wana ufanisi mkubwa. Wana washambuliaji wazuri na wanaweza kufunga hata katika hali ngumu kwa sababu wana kiwango cha juu.
''Tunapaswa kuhakikisha hatufanyi makosa. Lakini inatubidi kufanya kitu muhimu. Tunahitaji ukali, na sio makosa mengi. Tofauti kati ya Klabu Bingwa na Bundesliga ni kwamba wanakuadhibu kwa makosa yako.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment