Saturday, September 3, 2016
LIGI KUU YA UINGEREZA KAMA HOLLYWOOD ''NORDTVEIT''
Kiungo wa West Ham, Howard Nordtveit anafurahia kucheza katika ligi kuu ya Uingereza kama vile miugizaji mkuu katika filamu hollywood nchini Marekani. Kiungo huyo mweye umri wa miaka 26, alihamia London stadium kipindi hiki cha majira ya usajili akitokea Borrusia Monchengladbach na tayali ameshaonekana mara tano kweye kikosi cha hammers.
Nordtveit''alisema ninaishi maisha ya ndoto ya utoto wangu'' wakati nikiangalia ligi kuu ya uingereza na kuona wachezaji wakubwa wakicheza hapa na kuona maajabu yao nilikuwa nikijisikia raha na kutamani kucheza hapa ndoto ambayo imetimia''.
''Najisikia kama vile ulimwengu wote unakuangalia wewe kama vile uko hollywood'' ,pia Nordtveit alipingana na baadhi ya maoni ya watu kwamba amejiunga na West Ham kwa ajili ya maslahi zaidi, na ameripotiwa kuwa ni mchezaji kutoka Norway anaelipwa fedha nyingi zaidi kwa wakati wote ''sikuja hapa kwa ajili ya fedha lakini niko hapa sababu ilikuwa ndoto yangu na wamenitaka pia'' alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment