Sunday, September 25, 2016

ZVEREV AMALIZA MFULULIZO WA USHINDI WA KUMI NA MOJA KWA WAWRINKA FAINALI.


Alexander Zverev amemaliza ubabe wa bingwa wa US Open Stan Wawrinka wa muendelezo wa kushinda fainali ya kumi na moja, baada ya kumfunga kwa seti 6-2, 3-6, 7-5 kwenye fainali hizo za St Petersburg Open.
  
Alexander ambaye ni mtoto wa Profesa wa zamani Sir Alexander, ndio kwanza ana umri wa miaka 19 na kujishindia taji lake la kwanza la ATP World Tour baada ya kumfunga Wawrinka katika fainali hiyo ambayo inakuwa ya kwanza kwake kupoteza toka June 2013 alilpopoteza dhidi ya Nicolas Mahut kwenye Rosmalen Grass Court  Championships.  

Wawli hao waliingia fainali huku kila mmoja akiwa hajapoteza seti hata moja. Zverev anakuwa kijana wa kwanza kushinda taji hilo la ATP World Tour toka mwaka 2008 baada ya Cilic Marin aliekuwa na umri wa miaka 19 kushinda taji hilo kwenye michuano ya New Haven St Petersburg. 

No comments:

Post a Comment