Saturday, September 10, 2016

MACHO YOTE LEO ''MANCHESTER DERBY'' ENGLISH PREMIER LEAGUE



Licha ya leo kutakuwa na mechi nyingi zitazoendelea kwenye ligi mbalimbali duniani ,lakini karibi watu wote wanausubiria mchezo wa kusisimua kwenye Ligi Luu England.   

Leo hii ndio ile mechi ya kusisimu na iliyozungumziwa sana wiki hii ''Manchester derby'' watoto wa mji mmoja ambao ni mahasimu wakiwa chini ya makocha bora ambao pia ni wapinzani baada ya urafiki wao kuvunjika miaka iliyopita. Huku takwimu zikimbeba Guardiola dhidi ya Mournho kwani ameshinda mechi nyingi zaidi mbele ya mpinzani wake huyo toka waanze kukutana.     




Yamesemwa mengi lakini leo ni wakati wa dakika 90 kuamua nani mbabe kati yao kwenye mechi yao ya kwanza kukutana katika raundi ya nne ya Ligi Kuu, huku timu zote zikiwa na mwanzo mzuri wa ligi hiyo kwenye mechi zao tatu zilizopita. Huku mashabiki wa Man U wakiwaangalia nyota wao Ibrahimovic na Paul Pogba kuibeba timu yao.  


 Huku Man City wakimkosa mchezaji wao machachari Sergio ''Kun'' Aguero ambae anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu na FA, lakini wana David Silva na Rahim Sterling. Mechi hiyo kuchezwa  mchana wa leo saa 08.30. 

Ifahamike kuwa mchezaji wa Man U aliejiunga nao kwa uhamisho huru Zlatan Ibrahimovic ameshawai kuwa chini ya makocha wote wawili kwa kipindi tofauti na ligi mbili tofauti, ambapo aliwai kuwa chini ya Guadiola akiwa anaichezea Barcelona, katika La Liga.    
  

Na chini ya Mourniho akiwa Inter Milan katika ligi kuu ya Italia, Serie A.   


   

Mchezo hautabiriki kutokana na timu zote kutaka ushindi, ila baada ya dakika 90 tutajua nani mwamba.     
  
Pia michezo mingine itakayochezwa leo kwenye ligi hiyo ni pamoja na mechi ya West Ham vs Watford, Stroke City vs Tottenham Hotspurs, Middlsbourgh vs Crystal Palace, na Burnley vs Hull City, Arsenal vs Southampton, AFC Bournmouth vs West Brown, pamoja na Liverpool vs  Leicester City. Na kesho kutakuwa na mechi kati ya Swansea na Chelsea.    

 
  

No comments:

Post a Comment