Saturday, September 10, 2016
MATIC-UJIO WA KANTE ULINIFANYA NIWAZE KUONDOKA CHELSEA
Mchezaji wa kimataifa wa Serbia Nemanja Matic amesema aliangangalia nafasi yake ya baadae ndani ya Chelsea baada ya kuwasili kwa N'Golo Kante alietokea kwa Mabingwa wa Ligi Kuu Leicester City.
Anasema kuwa alifikiria kuondoka klabuni hapo kwani aliona kwamba pengine asingepata nafasi mbele ya Kante.''Kusema ukweli, niliongea na Conte,'' aliiambia SKY Sport, niliongea na klabu pia lakini pande zote tutakubaliana kwamba itakuwa vizuri kwa mimi kubaki. Na nina furaha sababu niko hapa klabuni pamoja na timu, na majukumu yangu kusaidia timu kupata ushindi kwenye mechi zetu za kupigania ubingwa.
Alihusishwa kuondoka na fununu zilisema kuwa angeenda Manchester United au Juventus. Kabla ajaamua kubaki Chelsea akiwa chini ya kocha mpya Antonio Conte. ''Alisema nina furaha kuwa hapa na ninahitaji kuinua kiwango changu na Conte ndie kocha sahihi wa kunisaidia kufanya hivyo.''
Chelsea watacheza ugenini dhidi ya Swansea jumapili hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment