Mahrez akishangilia na wachezaji wenzake wa Leicester City hapo jana
Kocha wa Leicester City Claudio Ranieri anaona kuwa kufunga kwao mapema kupitia goli la Albrington la dakika 5 na Mahrez dakika 29 kabla ya lile la dakika 61 la Mahrez kumeweza kuwafanya Mabingwa hao wa Premier League kuanza vizuri kwenye Champions League dhidi ya Club Brugge kwa ushindi wa 3-0.
''Ilikuwa ni muhimu kwetu kushinda baada ya kupoteza mchezo wetu uliopita dhidi ya Liverpool, tulifunga mapema mno na kutupa kujiamini zaidi,'' Ranieri aliiambia UEFA. Mabingwa hao wa Premier league walipoteza mchezo wao wa Europe kwa kufungwa 4-1 na Liverpool jumamosi iliyopita , na kwa matokeo hayo wameshuka hadi nafasi ya 16 katika meza.
''Club Brugge walicheza mpira vizuri, walitawala mpira lakini sisi tulitawala mechi na hilo ndilo lililokuwa zuri kwetu.''
''Inawezekana mwanzoni tuliwashangaza, niliwaambia wachezaji wangu kuwa mnaposikia muziki wa Champions League kuwa inajaza betri lako na kukufanya kupigana.''
Leicester ratiba yao ya pili kwenye kundi G watakutana na Porto Septemba 27.
No comments:
Post a Comment