Morata wapili kutoka kushoto akipongezwa na wachezaji wenzake wa Real Madrid
Alvaro Morata ameelezea kuwa alikataa nafasi ya kujiunga na Napoli kwa ajili ya kuithamini na heshima aliyokuwa nayo kwa Juventus.
Mhispania huyo amerejea Real Madrid akitokea kwa Mabingwa wa Serie A June mwaka huu baada ya kuamua kumrudisha kwa kumununu tena kwa euro million 30.
Juventus wameziba nafasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, kwa kuweka rekodi ya usajili klabuni hapo ya euro millioni 90 kwa Gonzalo Higuain, aliyefunga magoli 36 kwenye Serie A katika kuwania taji kwa mahasimu wao Napoli msimu uliopita.
Morata alidai kuwa alipokea ofa kutoka San Paolo lakini aliona kujiunga nao itakuwa kama vile usaliti kwa Juventus.
''Waliongea na wakala wangu, lakini sikufikiria kwenda huko kwa heshima ya Juve, ambao ninawachukulia kama familia yangu ya pili.'' alisema baada ya mpira kuisha ambapo alifunga bao la pili la ushindi kwa Madrid dhidi ya Sporting CP kwenye ushindi wa 2-1 kwenye Champions League, hapo jana.
''Juventus nao walileta ofa kubwa kwangu lakini Madrid walisema hapana, Juve ni klabu kubwa nchini Italia, lakini maisha yanaenda mbele na hamna anaejua kama katika siku zijazo njia yetu si kuvuka tena.''
Morata alifunga bao dakika za lala salama kipindi cha pili na kuipa Madrid pointi 3 kwenye mchezo waao wa kwanza katika makundi , baada ya Ronaldo kasawazisha dakika 89 baada ya Bruno Cesar's kuifungia bao la mapema Sporting CP.
Mpaka sasa ameshafunga mabao 2 katika mechi tano tangu aliporejea Santiago Bernabeu.
No comments:
Post a Comment