Monday, September 5, 2016
MATA AELEZEA HALI YA UTANI ILIYOPO KUELEKEA ''MANCHESTER'S DERBY''
Juan Mata amebainisha kuwa kumekuwa na utani unaoendelea ndani ya timu ya taifa ya Hispania baina ya wachezaji wanaotokea timu pinzani za jijini Manchester Uingereza, Man united na Man City. Kwamba kumekuwa na utani baina ya yeye na David De Gea wa Man U dhidi ya David Silva na Nolito wa Man City juu ya mechi yao ya ligi inayofatia baina ya timu hizo mbili za Uingereza.
''Mimi na De Gea tulikuwa tukiwatania Nolito na Silva juu ya mechi hiyo, ambayo sisi wote tunafahamu kwamba ni mechi muhimu kwetu, pia tunapaswa kuelewa kwamba hizi ni pointi tatu muhimu kwa kila timu''. Lakini sasa tunaangalia zaidi majukumu yetu ndani ya timu ya taifa.
Kiungo huyo wa United kwa sasa yupo kwenye majukumu na timu yake ya taifa ya Hispania akiwa pamoja na mchezaji mwenzake De Gea na wachezaji pinzani wa City Nolito pamoja na David Silva.
Hispania wameanza vyema kampeni yao ya kufuzu kombe la Dunia baada ya alhamisi iliyopita kuifunga Ubeligiji 2-0 kwenye mechi ya kirafiki. Vijana wa Julen Lopetegui wanacheza leo hii na Liechtenstein kwa ajili ya kuwania kufuzu kombe la dunia.
''Mata alisema, baada ya kumalizika kwa mechi za taifa, kuna mchezo jumamosi ijayo na nina uhakika unasubiriwa na wengi ''Manchester derby'', timu zote mbili zimeanza ligi vizuri na kila mmoja ana matarajio makubwa kama ambavyo kila mmoja anatarajia, baada ya hapo, tutakuwa na mengi ya kufikiria juu ya mchezo huo wa kusisimua''. Lakini hayo yote hayasumbui mawazo ya Mata kama ambavyo makocha Jose Mourinho na Pep Guardiola wanavyowaza kuendeleza upinzani uliopo baina yao. Baada ya hapo awali kuwa kwenye ligi moja ya Hispania.
Timu zote hizo zinazotokea jijini Manchester zimeanza ligi kuu ya Uingereza vizuri zote zikiwa na ushindi kwenye michezo yake yote mitatu iliyocheza, huku City akiongoza ligi kwa tofauti ya magoli.
Huku kukiwa na taarifa kuwa united ikikabiliwa na mtihani mzito kwenye safu yake ya ulinzi kuelekea mchezo huo wa ligi dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Manchester. Huenda wakawakosa mabeki wao wa pembeni Luke Shaw, ambaye alilazimika kusitisha mazoezi kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uingereza kama tahadhari baada ya kupata maumivu ya nyama za miguu, huku pia wakimkosa Antonio Valencia, ambaye atachelewa kurudi kutoka timu yake ya taifa ya Ecuador, ikiwa ni masaa 24 tu kabla ya mchezo huo kufanyika. Lakini united ambao washamkosa nyota wake muhimu Henrikh Mkhitaryan ambaye anauguza majeraha aliyopata wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Romania ilipokuwa ikicheza na Armenia.
United ina rekodi nzuri kwa msimu uliopita dhidi ya City ambapo walitoka suluhu bila kufungana Old Trafold na kupata ushindi wa bao 1-0 nyumbani kwa City Etihad Stadium bao hilo liliwekwa wavuni na Marcus Rashford.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment