Tuesday, September 6, 2016
YANGA WAIFUATA NDANDA MTWARA
Kikosi cha wachezaji 20 cha timu ya Yanga leo hii asubuhi kinatarajia kuondoka kuelekea mkoani Mtwara kwa ajili ya mchezo wake wa siku ya jumatano dhidi ya wenyeji wao,Ndanda FC.
Kikosi hicho cha kocha Mholanzi, Hans Pluijm kitashuka dimba bila ya wachezaji wake tegemeo sita, ambao wana udhuru tofauti, wachezaji hao ni pamoja kipa Deogratius Munishi ''Dida'' ambaye yupo kwenye msiba wa baba yake , mabeki Vincent Bossou ambaye yupo kwenye majukumu na timu yake ya taifa ya Togo, Pato Ngonyani, majeruhi na winga Geofrey Mwashuiya pamoja na kiungo Haruna Niyonzima ambaye pia yuko kwenye majukumu na timu yake ya taifa ya Rwanda na mshambuliaji Malimi Busungu ambaye ni majeruhi.
Na kikosi kitakacho safiri leo hii ni makipa wa timu hiyo Ally Mustapha ''Barthez'' na Beno Kakolanya, mabeki Juma Abdul, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji Mngwali, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Andrew Vincent ''Dante'' na nahodha Nadir Haroub ''Cannavaro'' pamoja na viungo Thabani Kamusoko, Obrey Chirwa, Said Juma, Simon Msuva, Deus Kasele, na washambuliaji ni Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Mathew Anthony.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment