Leo miamba miwili ya Ligi Kuu ya Serie A nchini Italia Internaziole Milan na Juventus inakutana katika uwanja wa San-Siro, mchezo huo unatarajiwa kuwa wa kusisimua baina ya pande zote mbili kuwa na upinzani mkali.
Huku kocha wa Juventus Massimilliano Allegri akiamini kuwa Derby d'Italia dhidi ya Inter Milan itafanya kugeukia mbio za kusaka ubingwa wa Serie A.
Inter Milan vs Juventus
Serie A
Sunday, September 18, 12:00 PM
San Siro
Inter Milan
|
vs
Juventus
|
Mechi hiyo inakuwa ya kwanza kuwakutanisha miamba hiyo ya Italia katika msimu huu wa 2016/17ambapo timu zote zina wachezaji wazuri.
Huku Juve ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja kati ya minne waliyocheza, wakishinda mitatu ya Ligi na kupata droo dhidi ya Sevilla kwenye Champions League. Huku vijana wa Frank De Boer, Inter wakishinda mchezo mmoja na kupokea kipigo kutoka kwa Itapoel Bee'r Sheva katika Europa League.
Allegri amesema kuwa utakuwa mchezo mzuri kwani watakuwa wanacheza na mahasimu wao na utawafanya kuelekea kwenye mbio za ubingwa.
''Mtu atazani kuwa tuko kwenye wiki ya mchezo wa nne, na sio kuwa katika maamuzi ya kuwania taji na sikubaliani na hilo.''
''Ni hatua yetu ya kwanza kugeukia mbio za ubingwa.''
No comments:
Post a Comment