Sunday, September 18, 2016

POGBA ANA KILA KITU-PEREYRA



Midfielder wa Watford Roberto Pereyra amemuelezea mchezaji mwenzake wa zamani wa Juventus Paul Pogba kuwa ana kila kitu.

Pereyra anaekutana na mfaransa huyo leo katika mechi ya Premier League itakayo zikutanisha timu hizo siku ya leo ambapo Man United watakuwa wageni kwenye mitaa ya Vicarage huku akijua kuwa anaenda kukutana na nani.

Wachezaji hao walikuwa pamoja Turin kabla ya wote kuhamia England kwenye majira ya usajili na sasa Pereyra ana matumaini ya kuwa mchezaji bora.   

''Ni mchezaji wa kizamani'' Pereyra aliwaambia The Guardian. 

''Ana kila kitu, ujuzi ambao huwezi kuufikiria ni mmoja kati ya wachezaji ambao huwezi kuwafikiria ambaye alinishangaza siku ya kwanza kumuona akicheza.''   

''Lakini tuko tayari kucheza  na kupigana na yoyote . Wote tunajua kuwa itakuwa ngumu lakini hili ni soka chochote kinaweza kutokea.'' 
 


No comments:

Post a Comment