Saturday, September 17, 2016

SIELEWI KWANINI SANCHEZ ALIPIGA PENATI ILE -WENGER




Baada ya kuibuka na ushindi wa 4-1 nyumbani kwa Hull City, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger hakujua kwanini Sanchez ndie aliepiga penati ambayo iliokolewa. Wenger amesema kuwa hakupanga Sanchez kupiga ile penati ila Santi Cazorla na haelewi kilichotokea hata ikawa hivyo.


Sanchez ambaye tayali jina lake lilikuwa kwa wafungaji na baadaye akaongeza bao la tatu, lakini golikipa wa Hull City aliokoa penati ya mshambuliaji huyo. Na Wenger alithibitisha kuwa Carzola yuko katika orodha ya wapigaji penati klabuni hapo.


 Magoli mengine kutoka kwa Walcott na Xhaka yaliwahakikishia ushindi kutoka KCOM na kuendeleza ushindi wao wa tatu kwenye mechi zao Premier League na Wenger alifurahishwa na kiwango cha timu yake. Lakini kwenye penati, Wenger aliiambia BBC Sport kuwa ''Cazorla ndiye aliekuwa tayali kwenda kupiga ile penati. Sielewi kilichotokea kwani hatukupanga Sanchez akapige ile penati.''


''Nahitaji kujua kilichotokea na sitopenda kijirudie tena. Kiujumla kila mtu anaweza kupoteza penati, inabidi tulikubali hilo. Inaweza kutokea kwa mtu yoyote yule na ingetokea hata kwa Cazorla pia.'' 


''Kiujumla kiwango kilikuwa kizuri baada ya kutoka kucheza Champions League, tulianza vyema na polepole, mchezo wetu ulikuwa fasaha na walituzuia vizuri na kutafuta nafasi za kutufunga lakini tuliweza kuwamudu na kuwafunga baada ya kukosa penati.''Hata hivyo ilikuwa kushindana na 11 kwa 10 aliongeza Wenger.


 

 

No comments:

Post a Comment