Sunday, September 18, 2016
MOURINHO ALIMTAKA LUCAS MOURA ALIPOKUWA REAL MADRID -WAKALA
Wakala wa mchezaji Lucas Moura ameweka bayana kuwa Jose Mourinho kipindi alipokuwa kocha wa Real Madrid alimtaka mchezaji huyo.
Lakini mchezaji huyo aliamua kujiunga na PSG na kuitosa Manchester United na mpaka sasa kocha huyo ameshatumia karibia Euro millioni 150 kwa msimu uliopita wa usajili.
Na hata sasa bado anamtaka ajiunge na Man United kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo.
Kipindi yuko Sao Paulo, Mbrazili huyo alikaribia kujiunga na Manchester United 2012 kabla ya kuamua kujiunga na PSG.
Wagner Ribeiro, amesema kuwa hata sasa kocha huyo wa United bado ana dhamira ya kumpeleka winga huyo Old Trafold baada ya kushindwa alipokuwa Real Madrid.
''Alisema kuwa aliyempigia simu Moura kwenda Madrid hakuwa Frolentino Perez bali Mourinho.'' Alisema wakala huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment