Monday, September 12, 2016

MOYES AOMBA UVUMILIVU KWA WAMILIKI SUNDERLAND


                                  Akitoa maelekezo kwa Donald Love wa Sunderland.

Kocha wa Sunderland David Moyes amewaomba wamiliki wa klabu hiyo kuwa wavumilivu dhidi yake na kumpa muda wa kuleta mabadiliko klabuni hapo.     

Moyes atawakaribisha timu yake ya zamani Everton kwenye uwanja wa Stadium of Light siku ya leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu.     

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 alitumia miaka 11 kuwa Goodison Park, ambapo alijenga uimara kwenye timu hiyo kiasi cha kuwapeleka kwenye michuano ya Europe licha ya kufanya kazi katika bajeti ya kawaida ya usajili. 

Toka aondoke Everton Moyes alidumu chini ya mwaka mmoja na  Manchester United kabla ya kutumia siku 364 akiwa na Real Sociedad ya Spain kama kocha.  

Huku akisisitiza kupewa muda zaidi na mabosi wa klabu hiyo kwani anaamini atafanya vizuri na Sunderland. 

Moyes alisema '' kama utaangalia vilabu vilivyokuwa na mafanikio utaona kuwa walikaa muda mrefu na makocha wao kama, Brian Clough alikuwa Nottingham Forest, nadhani kwa miaka 18, Sir Bobby Robson alikuwa Ipswich Town nadhani kwa miaka 13, Sir Alex Ferguson pia muangalie Arsenal Wenger na mimi pia''.  

Kama utaangalia muda mrefu wa makocha kuwepo kwenye vilabu vyao, utasema wamiliki wamewapa muda mrefu makocha wao ili kuweza kufikia kiwango cha mafanikio katika klabu zao. 

Moyes ambae hapo nyuma alikuwa Everton alifanya kazi na wamiliki wawili tofauti (Sir Philip Carter na Bill Kenwright), ambapo alisema wamiliki hao ingawa walikuwa na utawala tofauti lakini sababu ya vyombo vya habari na utofauti wao wa mashinikizo sababu ni wamiliki tofauti lakini walikuwa wakiona vile ambavyo timu wanataka iwepo.

Akiamini atafanya vizuri na klabu hiyo ya Sunderland na kuipa mafanikio kama aliyopata akiwa na Everton ambao alikaa nao kwa miaka 11. 
 

 
 

 

No comments:

Post a Comment