Thursday, September 15, 2016

NACHUKIA KUPOTEZA MECHI -COSTA




 Stireka wa Chelsea Diego Costa amesema kuwa anachukia kupoteza mchezo na kukubali kuwa inamchukua vigumu kutuliza hasira na hisia zake kwenye uwanja kama mambo yanapokuwa yameenda kinyume na anavyotaka.

Stireka huyo ambaye ameanza kwenye kikosi cha Blues kwenye mechi zote za Premier League amesema kuwa anapatwa na wakati mgumu sana anapotoka uwanjani akiwa katika hali ya huzuni.    

''Tunapoenda uwanjani tunataka kushinda, ndivyo tunavyohitaji kufanya. Na pale mchezo unapomalizika, kama umeshinda, unaenda nyumbani na furaha,'' Costa aliliambia jarida la Chelsea.
 
''Na ukipoteza mchezo, inakuwa ni picha tofauti mawazoni mwangu pale ninapomaliza mechi. Ninarudi nyumbani nikiwa nimekwazika. Kwa hiyo inatupasa kujua kuwa inabidi kuacha kila kitu uwanjani, kila tone la jasho ni kwa ajili ya kusaidia timu kushinda mchezo.    

''Sipendi kupoteza, sipendi kuwa kwenye eneo la kupoteza na nimeshaonyesha hilo mara nying tu. Na ninaonyesha hilo.         
 
''Nina amini kuwa hata wachezaji wenzangu wanajisikia hivyo ila kila mtu anaonyesha hisia zake kwa aina yake uwanjani na mimi ninakuwa na gadhabu nyingi kwenye kukataa kupoteza mchezo. Kila siku inabidi kuonyesha wewe ni wa aina gani uwanjani, na tayari nimeshaonyesha hisia zangu. 
 
 

No comments:

Post a Comment