Thursday, September 15, 2016

REKODI TANO MBAYA ZA LIVERPOOL DHIDI YA CHELSEA STAMFORD BRIDGES


Liverpool kuelekea mchezo wake wa kesho dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge kwenye mchezo wa Premier League tuangalie rekodi za Liverpool wakienda Stamford Bridge.   

Liverpool ambao wamewahi kushinda mara tu kwenye mechi zao tano za ugenini dhidi ya The Blue's, wametoka suluhu mara mbili na kufungwa mara mbili pia. 

 NOV11, 2012--Premier League
Luis Suarez anasawazisha goli kipindi cha pili kwenye mchezo mgumu waliotoka sare ya 1-1, wakiwa chini ya Brendan Rogers huku Chelsea wakiwa na kocha Roberto Di Mateo huku goli la Chelsea likifungwa na Johhn Terry kabla ya kutolewa nj'e akiwa majeruhi. 

DEC29, 2013--Premier League 
Kwenye mchezo huo Liverpool walifungwa 2-1 wakiwa na Roders tena huku Chelsea wakiwa na Jose Mourinho na magoli yakifungwa na Eden Hazard na Samuel Etoo, huku la Liverpool likifungwa na Martin Skrtel.

JAN 27, 2015--League Cup
Kwenye mchezo huu Chelsea walishinda f 1-0 kwenye dakika za nyongeza kwenye nusu fainali. Kwenye mchezo huo refa Michael Oliver alitoa kadi nane za njano  huku akikosa kuona makosa ya Diego Costa dhidi ya Emre Can ambaye baadaye alifungiwa mechi tatu. 

MAY 10, 2015--Premier League
 Steveni Gerald alifunga goli lake la mwisho dhidi ya Chelsea kabla ya kujiunga na LA Galaxy.              
Goli hilo lililofungwa na nahodha huyo liliwezesha Liver kutoka sare ya 1-1 na kipindi ambacho Gerald alitangaza kuondoka Liver na alitokea benchi dakika za mwishoni.            

OCTOBER 31, 2015--Premier League
Jurgen Klopp anapata ushindi wake wa kwanza kwenye premier League kama kocha mpya kwenye ushindi wa 3-1 Stamford Bridge huku kukiwa na hofu ya vijana wa Mourinho kuendeleza historia yao kwa Liver baada ya Ramires kuifungia Chelsea goli la kuongoza kabla Countinho kumaliza uteja wao.
  


 
 

No comments:

Post a Comment