Saturday, September 17, 2016

NYIMBO YA CHAMPIONS LEAGUE ILIMUAMSHA MAHREZ -RANIERI


Kocha wa Leicester City Claudio Ranieri amesema kuwa nyimbo ya Champions League ilimuamsha mchezaji wake Riyad Mahrez aliyefunga magoli mawili katika mchezo wao uliopita wa siku ya Jumatano dhidi ya Club Brugge kwenye Champions League.  


''Ilikuwa ni vizuri sababu alifunga mara mbili, ukijumlisha na free-kick yake nzuri, na anafanya kazi kwa bidii.'' alisema kocha huyo wa Foxes. 

''Pengine alishachoka na kusikiliza kengere zangu ninazo wapigia muda wote,'' aliongezea Ranieri.''  

''Sasa tunahitaji kutulia na kupeleka mawazo yetu kwenye mchezo wetu wa leo dhidi ya Bunley kwenye Premier League. Wapinzani wetu  watataka kutufunga kwa kufikiria kuwa tumechoka, lakini siamini hilo. 

Mahrez ambaye amefunga goli moja katika michezo yake minne ya Premier League aliibuka shujaa kwa Leicester kwenye mchezo wao wa kwanza katika makundi kwenye Champions League.    
 

No comments:

Post a Comment