Thursday, September 15, 2016

UINGEREZA KUWAVAA ARGENTINA NUSU FAINALI DAVIS CUP


Mcheza tenisi namba mbili kwa ubora duniani upande wa wanaume Andy Murray na timu ya Uingereza ya tenisi wako tayari kwa ajili ya msukumo mkubwa zaidi wiki hii ambapo watajaribu kutetea taji lao la ubingwa kwenye nusu fainali ya Davis Cup. 


Uingereza watacheza na Argentina, Glasgow siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, na mchezaji huyo namba mbili kwa ubora duniani ana matumaini ya kutetea taji hilo baada ya kuiongoza timu hiyo mwaka jana na anatumainiwa kufanya hivyo pia mwaka huu.Huku akimsifia mchezaji wa Argentina Juan Del Porto kuwa ni mchezaji mzuri duniani kwa sasa kwenye mchezo huo.     

Alisema kuwa ''tunaitaji kujaribu kufanya tena mwaka huu kama itawezekana. Inaelekea kuwa ngumu lakini ninachotaka ni kushinda michezo yote, ninahitaji kujaribu kumaliza mwaka nikiwa imara kadri niwezavyo.''        

Pamoja na uchovu wa mapumziko aliokuwa nao na kufikia fainali ya French Open na kumuona akishinda kwa mara pili kombe la Wimbledon na kurudisha taji lake la Olimpiki, na kupoteza US Open dhidi ya Kei Nishikori kwenye hatua ya robo fainali.   

''Umekuwa ni mwaka mzuri kwa kazi yangu, hivyo nina matumaini ya kuendelea kufanya vizuri zaidi,'' aliongezea Murray.  

Croatia atakutana na Ufarans kwenye nusu fainali nyingine Zadar. 

  

 

No comments:

Post a Comment