![]() |
| Pogba akifunga bao lake kwa United toka ajiunge nao. |
Magoli manne ya haraka ndani ya kipindi cha kwanza yaliweza kuisadia Manchester United kutoka kifua mbele dhidi ya Mabingwa watetezi wa Premier League wa msimu uliopita Leicester City ndani ya dimba la Old Trafford.
Huku nyota wao waliomsajili kwa gharama iliyovunja rekodi Paul Pogba akiwa mmoja kati ya wafungaji hao.
Alikuwa Chris Smilling alienza kuzifumania nyavu za mabingwa hao kwa goli lake la dakika 22, Juan Mata akawanyanyua tena mashabiki wa United vitini kwa goli lake la dakika ya 37, huku kinda anaetengeza rekodi ya kufunga kila mechi Marcus Rashford akitupia goli la tatu ndani ya dakika ya 40, kabla ya Pogba kuhitimisha kalamu hiyo ya magoli kwa United dhidi ya Leicester ndani ya dakika 42 na kufanya kipindi cha kwanza kikimalizika kwa vijana wa Mourinho kuwa mbele kwa 4-0. Ambapo Leicester walipata goli lao la kufutia machozi kupitia Demarai Gray ndani ya dakika ya 59 ya kipindi cha pili.
Kabla ya mechi hiyo kuanza Mourinho aliiambia Sky Sports kuwa amewachagua Rashford na Lingard kuanza dhidi ya Wayne Rooney, sababu mchezo utakuwa wa haraka kwa aina ya uchezaji wanaocheza na jinsi wanavyo nyoosha mchezo ,huku mshambuliaji mkuu Ibrahimovic akihitaji watu wenye spidi kumzunguka ili kuleta morali kali ya mchezo. Wayne rooney aliingia kipindi cha pili cha mchezo huo ndani ya dakika ya 83 akibadirishana na Rashford alietolewa.

No comments:
Post a Comment