Friday, September 23, 2016

ROONEY NI BINGWA LAKINI HAWEZI KUWA UPANDE WANGU-RANIERI


Kocha wa mabingwa wa Premier League msimu uliopita Leicester City Claudio Ranieri amesema kuwa Wayne Rooney hawezi kuwa katika timu yake.
Licha ya kumuita ''bingwa'' nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Uingereza, Ranieri alisema kuwa anafuraha na washambuliaji wake katika timu yake na hana mpango wa kubadirishana na mchezaji yoyote wa Man United. 

Rooney ambaye ana hali ngumu kutoka kwa mashabiki na halio hiyo huenda ikamfanya Jose Mourinho kutomchezesha dhidi ya Leicester.  

Ranieri alisema ni mchezaji mzuri na bingwa, lakini nawapenda wachezaji wangu, na sitoweza kuwabadirisha na mchezaji yeyote.'' 

No comments:

Post a Comment