Saturday, September 24, 2016

VPL YAENDELEA LEO HUKU SIMBA IKITUMA SALAMU YANGA, YAIPIGA MAJIMAJI 4-0


Mnyama leo ameibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Majimaji kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwenye uwanja wa Taifa.
Huku magoli ya Simba SC yakifungwa na jamali Mnyate dakika ya 4 ya mchezo huo kipindi cha kwanza na goli hilo lilidumu mpaka kipindi cha pili, kabla Kiza Kichuya kuipatia Simba goli la pili kwa njia ya penati dakika ya 66 baada ya mchezaji wa Majimaji kuunawa mpira na mwamuzi kuamulu penati na Mnyate tena akawanyanyua vitini mashabiki wa Simba SC kwa goli lake la dakika ya 75 kabla ya Kichuya kuitimisha idadi ya magoli kwa Simba kwa goli lake la dakika ya 81.

Huku Azam akiwa mgeni akapokea kichapo toka kwa Ndanda katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, na kwa matokeo hayo Azam anapoteza mechi yake ya pili baada ya kwanza kupoteza dhidi ya Simba SC. 

Huku JKT Ruvu akiwachezesha gwaride Mbeya City baada ya kuwapa kipigo cha 2-0 kwenye mechi iliyochezwa uwanja wa Mabatini mkoani Pwani. 

Pia Mtibwa Sugar ikitoka sare dhidi ya Mbao FC  nyumbani kwao Manungu, Morogoro.Huku Mtibwa wakiwa wakwanza kufunga goli hilo kabla ya goli la jioni la Mbao lililowafanya wagawane pointi.

No comments:

Post a Comment