Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, imeendelea wikiendi hii kwa michezo mbalimbali kuchezek hapo jana na leo hii na mchezo mwingine unatarajiwa keundelea kesho kati ya African Lyon dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa Uhuru.
Hapo jana mabingwa wa Ligi hiyo Yanga Afrika walikuwa wenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye uwanja wa Uhuru, na Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 yaliyofungwa na mfungaji bora wa Ligi msimu uliopita Amissi Tambwe aliefunga 2 na na kiungo Deus Kaseke aliefunga 1, vile vile kulikuwa na mchezo kati ya Azam FC na Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya ambapo Azam ikishinda goli 2-1.
Pia Mkoani Shinyanga kulikuwa na mchezo kati ya Mwadui FC na Stand United kwenye uwanja wa Mwadui Complex ambapo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, nayo Ndanda FC ikiwa wenyeji wa Kagera Sugar walitoka sare ya 0-0 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona na Ruvu Shooting waliwafunga wapinzani wao JKT Ruvu bao 1-0.
Na leo ''Mnyama'' Simba SC alikuwa akicheza na mgeni wake Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye uwanja Uhuru na kuifunga goli 2-0, mabao yaliyofungwa na Ibrahim Ajib dakika ya 52 na lapili likiwekwa wavuni na Mavugo dakika ya 66 na kuifanya Simba iondoke na pointi 3 muhimu.

No comments:
Post a Comment