Leo kulikuwa na mechi ya hisani ya wabunge wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kwa ajili ya kuchangia waarithika waliopata tetemeko la ardhi mkoani Kagera ambao wana hali mbaya ya kimaisha.
Mechi hiyo iliwakutanisha wabunge mashabiki wa Simba na mashabiki wa Yanga, ambapo wabunge mashabiki wa Yanga walifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya wabunge mashabiki wa Simba na mchezo huo ulichezwa kwa dakika sitini.
Wabunge mashabiki wa Yanga waliweza kufunga mabao yao haraka haraka ndani ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo uliokuwa umejaa burudani za aina zake katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Ambapo mabao ya wabunge hao mashabiki wa Yanga yakifungwa na Sadifa Juma, Mohamed Mchengerwa dakika ya (3,8), na Mwigulu Nchemba dakika ya (25,28), huku ya Simba yakifungwa na Cosato Chumi dakika ya 18 na Yusufu Kaiza aliefunga kwa mkwaju wa penati.
Yanakuwa matokeo mabaya kwa Yanga ambao Jumamosi ijayo wanacheza na watani wao wa jadi Simba SC ambao walipata matokeo mazuri kuelekea mchezo huo.

No comments:
Post a Comment