SIMBA NA AZAM ZATAKATA VPL, YANGA HOI MTWARA
Hapo jana jumatano,07/09/2016 kulikuwa na michezo mitatu ya ligi kuu ya Vodacom, ambapo timu ya Simba ilishuka dimbani dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, ambapo Simba wakitoka nyuma ya bao 1 na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wageni wao Ruvu Shooting, kupitia mabao ya Hajib na Mavugo timu hiyo ilifanikiwa kuondoka na pointi 3 muhimu huku lile la Ruvu likifungwa na Abdulrahman Mussa.
Napo kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ambapo Azam ilicheza na Prisons, timu ya Azam ilifanikiwa kushinda bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao hao.
Na huko mkoani Mtwara, mabigwa wa ligi hiyo Yanga wameshindwa kuvunja rekodi ya kuifunga Ndanda kwenye uwanja wa nyumbani Nangwanda Sijaona baada ya kulazimishwa sare ya 0-0. Huku Ndanda wakiendelea kulinda rekodi yao dhidi ya Yanga kwenye uwanja huo mkoani Mtwara.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii.
No comments:
Post a Comment