Tuesday, September 20, 2016

YAMETIMIA KILIMANJARO QUEENS MABINGWA KOMBE LA CECAFA 2016.



Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara''Kilimanjaro Queens'' wamekuwa Mabingwa wa kwanza wa Kombe la CECAFA Chalenji kwa wanawake, baada ya kuifunga Kenya 2-1 katika Fainali iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Ufundi,Njeru jijini Jinja. 

Mabao ya Mwanahamisi Omari ya kipindi cha kwanza yaliweza kuzima ndoto za Kenya ambao pia wamefuzu kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika ikiwa ni timu pekee kwa upande wa CECAFA.

Kilimanjaro Queens walianza vyema michuano hiyo kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Rwanda, na kuja  kuwafunga wenyeji Uganda kwenye Nusu Fainali 4-1 na kutinga Fainali ambayo wanarudi  nyumbani na Kombe hilo kama ambavyo kocha wao alivyoahidi ushindi kwenye Fainali siku ya leo.     

No comments:

Post a Comment