![]() |
| Bailly akishindwa kuendelea na mchezo. |
Madaktari wamethibitisha kwamba beki wa Manchester United raia wa Ivory
Cost Eric Bailly atakuwa nje kwa muda wa miezi miwili kufuatia majeraha
ya goti aliyopata Jumapili hii kwenye mchezo wao dhidi ya Chelsea
Stamford Bridge ambapo ''The red devils'' walipata kipigo cha mabao 4-0
Beki
huyo alilazimika kutolewa nje dakika ya 52 baada ya kuumia na leo hii
ameposti picha inayomuonyesha mguu wake ukiwa na kifaa maalumu cha
kumsaidia kutembea pamoja na kupona haraka.
![]() |
| Bailly akiwa na kifaa kinachomsaidia kutembea baada ya majeraha. |
Bailly ambaye alijiunga na United akitokea Villarreal kwa uhamisho wa paundi miliion 30 msimu huu, kukaa kwake nje kunakuwa pigo kwa Jose Mourinho ambaye kikosi chake kinatabu kwenye upande wa mabeki.
Beki huyo alisema,
''Ninawashukuru kwa ujumbe mliokuwa mnanitumia kipindi chote toka niumie,'' aliandika kupitia mtandao wa instagram.
''Nina matumaini ya kucheza tena United na The Elephants kabla ya miezi miwili, kwa uweza wa Mungu. Asantewa kuwepo hapa.
Beki huyo pia anatarajiwa kuwepo kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika January mwakani.


No comments:
Post a Comment