![]() |
| Kuznetsova akikata nywele zake kwenye fainali za WTA. |
Mchezaji namba 9 kwa ubora duniani kwenye mchezo wa tenisi Svetlana Kuznetsova amelazimika kukata nywele zake alizokuwa amezibana wakati wa mchezo wa fainali za WTA nchini Singapore dhidi ya Agniezska Radwanska. Mchezaji huyo alimuomba mwamuzi mkasi ili aweze kupunguza mkia wa nywele zake zilizokuwa zikimpa tabu wakati wa fainali hizo ambazo aliibuka mshindi.
Kuznetsova ambaye alionekana mchovu wakati wa seti ya mwisho wa mchezo huo, lakini aliweza kurudi kwenye hali yake ya kawaida ya kimchezo na kuweza kumaliza akiwa na machozi ya furaha.
Aliweza kurudisha hali ya utulivu na kufanya mabadiriko kwenye seti hiyo ya mwisho kwa 7-5.
![]() |
| Kuznetsova akishangilia ushindi wake. |
Mchezaji huyo aliweza kuelezea jinsi ambavyo mkia huo ulivyokuwa unampa tabu kipindi cha mchezo.
''Ulikuwa ukinikera sana. Nilikuwa kila mara nikijaribu kuweka kwenye mkanda wa nywele, lakini nywele zangu ni nzito na nene sana.'' Alisema .
Mchezaji huyo ambaye alisema kuwa wakati ambao alikuwa akijaribu kupiga mpira alikuwa akipata shida na mkia huo ulikuwa ukimpiga jichoni hali ambayo ilikuwa ikimpa tabu, pia aliongezea kuwa
''Nilifikiria kuwa sawa!, nini muhimu sasa? Nwele zangu ambazo niziache kukua au mechi? Nikafikiria kuwa SAWA ninahitaji kufanya uamuzi sasa hivi na ikawa hivi.''
Mchezaji huyo sasa atakutana na karolina Pliskova Jumatano.


No comments:
Post a Comment