Monday, October 17, 2016

BEGA LAMUWEKA NJE SERENA FAINALI ZA WTA SINGAPORE.

Serena Williams akishangilia taji lake la Wimbledon.
Serena Williams amejitoa kwenye fainali za mwisho za WTA kufuatia majeraha ua bega aliyopata, mchezaji huyo namba  mbili kwa ubora wa mchezo wa tenisi amesema leo hii.
 
Bingwa huyo mara mbili wa Grand Slam amecheza mashindano nane na kupoteza kwa Mjerumani Angelique Kerber.

Serena alisema ''umekuwa mwaka mbaya kwangu kukabiliana na majeraha ya bega. Daktari wangu amesisitza nikae nyumbani ili niweze kupona majeraha hayo. Nitakuwa na kumbukumbu nzuri juu ya Singapore na kusema ukweli nitawakumbuka mashabiki wangu. Alisema mchezaji huyo mwenye miaka 35. 

Mcheazji huyo maarufu wa tenisi anauguza jeraha lake toka mara mwisho aliposhinda Wimbledon. 



 

No comments:

Post a Comment