Monday, October 17, 2016

CLAUDIO BRAVO NA MTIHANI WA KUWAKABILI MSN.

Claudio Bravo, golikipa wa Manchester City.
Uamuzi wake wa kuachana na Barcelona haukuwa mbaya kwake kwani kujiunga kwake na Manchester City kumeweza kumfanya kuingia kwenye orodha ya magolikipa bora kwa siku za usoni.

Bravo ambaye Jumatano hii anarudi Nou Camp kwenye mchezo wa kundi C kwenye Ligi ya Mabingwa akiwa na Man City itakayo pambana na Barcelona kwenye mchezo wa makundi.

Bravo ambaye ameweka wazi kurejea kwake Nou Camp na mtihani wa kuwakabili MSN lakini akionyesha kujiamini na kusisitiza atafanya awezalo kuhakikisha ubora wake unakuwa mzuri dhidi ya mchezo huo.  Aliwaambia MARCA kwamba ''Ninarejea nikiwa na amani ya mawazo na matamanio ya kucheza mchezo mzuri, nitafanya kama nilichotakiwa kufanya (Barcelona) na nina furaha kurudi Blaugrana kwenye hatua kubwa ya soka duniani.'' 

''Kuwakabili MSN ni mtihani mkubwa sababu ni wachezaji wazuri, lakini kucheza kwetu vizuri kutaweza kuwadhibiti.

''Kama Lionel Messi ni mchezaji wa ajabu, na anaefanya mabadiliko muda wowote.''  

Bravo ambaye alikuwa Barca msimu uliopita aliondoka Nou Camp kutokana na kukosa nafasi za kucheza klabuni hapo na kujiunga na  Man City. 


No comments:

Post a Comment