![]() |
| Rais wa ufaransa Francois Hollande. |
Lile sakata linaloendelea kati ya wachezaji wawili wa timu ya taifa ya Ufaransa kati ya Karim Benzema na Mathieu Valbuena juu ya mchezo mchafu uliofanywa na Benzema juu ya kanda chafu ya mchezaji mwenzake, imepelekea rais wa Ufaransa Francois Hollande kuingilia suala hilo ambalo toka kadhfa hiyo itokee imemfanya Benzema kuwa nje ya kikosi cha Les Blues.
Huku Benzema akiendelela na majukumu yake ndani ya kikosi cha Real Madrid tena akiwa na kiwango kikubwa lakini Les Blues wamekuwa wakimkacha kwenye mechi zao za taifa.
![]() |
| Karim Benzema. |
Hollande alisema kupitia kwenye kitabu chake kwamba ''Kimaadili Benzema sio mfano wa kuigwa.''
''Timu ya taifa ya Ufaransa inapaswa kutoa mafunzo kidogo ya uwanjani na kutoa zaidi kwenye misuli ya ubongo,'' aliongeza rais huyo.
''Hakuna jamii ndani ya timu ya taifa ya Ufaransa, hakuna muambatano kati ya klabu na nchi. Katika timu kuna watu kutoka maeneo masikini sana ambayo waliyooacha ili kucheza mpira nje.
Inatokana na wafatiliaji na idadi kubwa ya maoni juu ya jinsi ya kukabiliana na matatizo ya soka la kisasa.


No comments:
Post a Comment