![]() |
| Karim Benzema. |
Ikiwa zimepita siku chache toka rais wa Ufaransa Francois Hollande ampige dongo kwenye kitabu chake mshabuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufarasa Karim Benzema, na sasa mshambuliaji huyo amejibu mapigo kwa rais huyo.
Benzema ambaye hakuwepo kwenye kikosi cha Ufaransa kilichocheza Euro 2016, kufuatia mashtaka yanayomkabili juu ya kuhusika kwenye kumlaghai mchezaji mwenzake Mathieu Valbuena juu ya mkanda wa mapenzi.
Hollande ambaye ndani ya kitabu hicho kijulikanacho kama ''A President Shouldn't say that.'' Ambapo ndani ya kitabu hicho alieleza kwa ujumla na kukosoa akili za wachezaji wa Ufaransa na kusema kwamba kimaadili Benzema sio mfano wa kuigwa.
Nae mchezaji huyo baada ya jana kuweza kuisadia klabu yake ya Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 50 dhidi ya Legia kwenye klabu ya Mabingwa.
''Unataka mimi niseme nini? Kwamba sio mfano wa kuigwa? Benzema alinukuliwa na Le Parisien.
''Ninacheza mpira, nafanya watu waburudike wenyewe na nimesomeshwa vizuri na wazazi wangu.''
Pamoja na kiwango chake kizuri ndani ya Madrid lakini kocha wa timu hiyo Didier Deschamps hajamuita kwenye kikosi kinachowania kufuzu Kombe la Dunia.
''Timu ya taifa? kwa kweli naona.'' Mchezaji huyo wa zamani wa Lyon aliongezea.
''Hakuna sababu inayonifanya niongelee hilo muda wote. Ninahitaji kuwa makini juu ya uwezo wangu klabuni.''
Benzema ambaye ana matumaini ya kupokea simu juu ya kuichezea timu ya taifa tena lakini akiwa hatarajii suala hilo kumuumiza akili yake alisema ''kwangu, jambo la muhimu kurudi kuichezea Ufaransa, ni hayo tu.''

No comments:
Post a Comment