![]() |
| Lionel Messi. |
Mshambuliaji wa Manchester City Nolito amemsifia nyota wa Lionel Messi kwamba wa tofauti kwenye ushindi wa Barcelona 4-0 dhidi yao kwenye Ligi ya Mabingwa.
Messi ambaye kwenye mchezo huo alifunga hat-trick kabla ya Neymar kuhitimisha kalamu hiyo ya mabao kwenye uwanja wa Nou Camp.
Kwenye mchezo huo hapo jana golikipa wa Man City Claudio Bravo alitolewa nje na huku pia Jeremy Mathieu wa Barca akipewa kadi nyekundu na Neymar akikosa penati.
Nolito alisema ''Messi ni mchezaji bora duniani, hivyo hufanya tofauti.'' Aliongea kupitia tovuti ya klabu yao.
''Pale anapokuwa na mpira siku zote atafanya kitu, goli au pasi.''
Kutolewa nje kwa Bravo kuliweza kuigharimu timu hiyo kwani baada ya kipa huyo kutoka ndipo udhaifu wa Man City ulionekana. Nolito ambaye anaamini kuwa walicheza vizuri lakini hawakuwa na bahati kwenye mchezo huo.
''Tulicheza vizuri kwenye kipindi cha kwanza, tulikuwa na nafasi lakini kipindi cha pili hatukuwa na bahati.
''Huu ni mpira lakini, tunahitaji kusonga mbele. Leo ilikuwa ngumu kupambana na Barcelona, lakini hatukustahili kupoteza kwa 4-0.''

No comments:
Post a Comment