![]() |
| Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antonie Griezmann. |
Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antonie Griezmann anajisikia kushinda mataji zaidi ili aweze kufanana na wachezaji wawili wanaopishana kuchukua tuzo ya Ballon d'Or Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, lakini shauku yake hiyo haimfanyi kuhama klabu yake ya Atletico ili kuweza kufikia lengo hilo.
Mfaransa huyo amekuwa akizungumziwa juu ya kuweza kushinda tuzo hiyo baada ya kiwango chake kizuri kwa msimu uliopita na msimu toka uanze mwaka huu, pamoja na kuzungumziwa huko lakini Mfaransa mwenzake Franck Ribery amesema kwamba mshambuliaji huyo mwenye miaka 25 bado hajafikia uwezo wa kuchukua tuzo hiyo.
Hata hivyo Griezmann alikubali kwamba bado ajafikia kiwango cha nyota wa Barcelona na Real Madrid, lakini aliweka wazi kwamba atafanya kila awezalo hata kwa kutumia nguvu aweze kufikia kiwango cha wachezaji hao.
''Sijisikii kuwa niko kwenye kiwango cha Messi na Ronaldo bado kwa kweli, nahitaji kushinda mataji ili niweze kufanana nao. Ninajaribu kusaidia timu yangu na nchi yangu kwa kila zuri ninaloweza kufanya,'' aliiambia Eurosport.
''Ninajisikia faraja pale Simione anaponiambia kwamba ninaweza kufikia kiwango cha Messi na Ronaldo. Siku zote nahitaji kumpa vyote niwezavyo, ananihamasisha. Nina furaha na kocha wangu anadhani ninaweza kufikia kiwango chao.
''Ninahitaji kulithibitisha hilo kwa kile nilichofanya msimu uliopita. Griezmann aliongezea kwamba ''watu wanaongea juu ya Barca na Madrid na kuisahau Atletico, lakini kwangu jambo kubwa ni kile kinachotokea uwanjani. Tunashindana nao mwaka baada ya mwaka, Sivutiwii na sifa ya klabu.
''Ballon d'Or? hiyo ni juu ya waandishi wa habari kupiga kura. Kila usiku sipandi kitandani nikifikiria juu ya hilo. Ninachofanya ni kufanya niwezalo na kufunga mabao mengi kila niwezapo.''

No comments:
Post a Comment