Monday, October 31, 2016

BONAVENTURA AWAPA ZAWADI BAO LAKE WAHANGA WA TETEMEKO LA ARDHI.

Mchezaji wa AC Milan Giacomo Bonaventura amewapa bao lake alilofunga kwa AC Milan 1-0 dhidi ya Pesara kwenye Serie A kwa wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea katikati ya Italy. Mji wa Norcia uliweza kukumbwa na shambulio hilo lililokuwa na ukubwa wa 6.6 Jumapili.  Tetemeko hilo ambalo ni kubwa kuwahi kutokea nchini Italy toka mwaka 1980 limeharibu majengo mbalimbali , na watu takribani 20 wamejeruhiwa.
Ilizaniwa kwamba hakutakuwepo na tetemeko baada ya lile la mji wa Amatrice lililoharibiwa kwa kiwango cha ukubwa 6.2 mwezi Agosti na kuwaacha watu 297 wakiwa wamekufa, huku mikoa ya Marche na Umbria ikizaniwa kuwa na ukubwa wa kipimo cha tetemeko kama litatokea.

Bonaventura ambaye amezaliwa San Severino Marche, aliposti kipande cha video kilichobeba ujumbe kwa wahanga hao wa tetemeko ''Forza Italia'' baada ya kufunga bao kwenye uwanja wa  Pescara.

''Nalitoa hili goli kwa watu waliopatwa na tetemeko la ardhi,'' alisema Bonaventura.

''Ninajua kwanini sababu mimi ninatokea sehemu hizo.

''Ninawatumia kumbatio kubwa na ninajua tutafanya kitu kitakachopangwa kama timu kuwasaidia.''

Kwenye ushindi huo vijana wa Vicenzo Montellas umeweza kuwapandisha mpaka nafasi ya tatu  kwenye Serie A, Bonaventura alisema ''nina furaha kwa ushindi. Tulipata shida lakini jambo jema ilikuwa kushinda. 

No comments:

Post a Comment