Monday, October 31, 2016

GRIEZMAN BADO ANA MATUMAINI YA KUSHINDA BALLON d'OR.

Mtu aliyevumbua kipaji cha mchezaji Antoine Griezmann amesema kwamba Mfaransa huyo bado ana matumaini ya kushinda Ballon d'OR, Eric Olhats ambaye alivumbua kipaji cha nyota huyo wa Atletico Madrid  akiwa na miaka 14 ambaye toka kipindi hiko alikuwa chini yake na akimuangalia alipokuwa Real Sociedad, hajakata tamaa ya kuwapiku nyota Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kutajwa kuwa mchezaji bora wa dunia.
Griezamann ambaye ameshinda kiatu cha dhahabu kufuatia mabao yake sita kwa timu ya taifa ya Ufaransa kwenye Euro 2016 na kuisaidia Atletico Madrid kumaliza nafasi ya tatu LaLiga.

Mara ya mwisho kwa mchezaji mwingine kushinda tuzo hiyo ilikuwa mwaka 2007, pale kiungo wa Brazil Kaka aliposhinda tuzo hiyo, na Ohlats amesema kwamba tuzo hiyo inakweza kuwa ya Griezmann kwa mwaka 2016.

Ohlats aliiambia L'Equipe ''Antoine ana matumaini kwamba waandishi wa habari watapiga kura na sababu ya kuwa imara zaidi kwa orodha ya wachezaji kwenye orodha yao ya kila mwaka.

''Bahati nzuri, kuna vigezo vingine ambavyo viko kwenye kucheza, kama maendeleo ya mtu binafsi.

''Kutoka hapo tunaweza kudhani kwamba ana nafasi. Griezmann kamwe hakati tamaa.

No comments:

Post a Comment