Sunday, October 30, 2016

GUARDIOLA ANALIPIZA KISASI KWA TOURE- WAKALA

Guardiola akitoa maelkezo kwa Yaya Toure.
Wakala wa mchezaji raia wa Ivory Coast Yaya Toure, Dimitri Seluk amesema kwamba meneja wa Manchester City Pep Guardiola analipa kisasi kwa Yaya kwa kumuweka nje ya kikosi chake. Kumekuwa na mgogoro unaoendelea kati ya wakala wa Yaya Toure na Pep Guardiola kufuatia wakala huyo kutoa maneneo ya hasira kwa kocha huyo wa City baada ya mchezaji kutocheza ndani ya kikosi hicho ambacho Yaya mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa mwezi Agosti kwenye mechi ya Klabu ya Mabingwa kati ya City dhidi ya Steau Bucharest.
 Wakala huyo anasisitiza kuwa ugomvi huo unatokana na kipindi ambacho Pep alikuwa Barcelona 2010 na kumuuza Yaya kwa Man City kwa uhamisho wa euro million 24 ambapo yeye alimkosoa Pep juu ya uhamisho huo.

 
Dimitri Seluk wakala wa Yaya Toure.
Seluk alisema ''najua tatizo lake ni wakati ambao Pep alikuwa hamtaki Yaya kuwepo Barcelona mimi nilimkosoa juu ya hilo.

''Hiki ni kisasi chake na wala sio utaalamu.''

''Niliwauliza City kwenye majira haya ya uhamisho kama walitaka Yaya aondoke lakini walinijibu kuwa yuko kwenye mipango yao.''

''Wakati ambao Yaya aliachwa kwenye kikosi cha Champions League, nilimpigia Pep. Nilitaka kujua sababu zake juu ya kufanya hivyo lakini hakunipigia.'' Aliongezea Seluk.

''Nikajaribu kumpigia Txiki , lakini nae hakunipigia pia. Kwahiyo sizani kama klabu inaweza kunikosoa kufanya mahojiano na magazeti huku wakiwa hawataki kuongea na mimi.

''Pep anaongea kuhusu heshima. Lakini kupata heshima unapaswa kuionyesha,. Kabla Citu haijacheza Nou Camp , nilimpigia simu Pep tena. Nilitaka kumuuliza kama tutaonana wakati amabao yuko Barcelona.

''Pia nikampigia Txiki, lakini hakuna lolote lililokuja. Nikawatumia mesage pia. lakini tena hakuna chochote kilichorudi. Nina rekodi za simu zote kwa ushahidi zaidi.''
Seluk alisema kwamba ''sikuwa na nia ya kufanya mawasiliano ya kuomba msamaha kwani Pep na Txiki wanajua hilo. Kwanini niombe msamaha nikiwa sina hatia yoyote zaidi ya kuogea ukweli?

''Mawazo yangu yalikuwa kuongea kiume, kutafuta njia itakayoweza kuwa bora kwa faida ya Man City na Yaya. Lakini nilichopata ni ukimya .Kwahiyo ni dhahiri kwa kila mtu kwamba Pep hataki msamha.

''Ni wakati wa kumgeukia Sheikh Mansour na mashabiki wa City  dhidi ya mchezaji wanaempenda.

''Pep anaruhusu hasira yake kufanya maamuzi ambayo sio bora kwa  Manchester City.''



















No comments:

Post a Comment