Sunday, October 23, 2016

GOR MAHIA WAFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA LIGI KUU KENYA.


Timu ya Gor Mahia wamejihakikishia matumaini yao ya kushinda taji la ligi ya Kenya baada ya kuwashinda wapinzani wao jadi AFC Leopard 2-0 katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi. Ni mechi iliyokuwa na upinzani mkali na mashabiki wengi walijitokeza siku ya leo Jumapili kwani mashabiki wa Green Army na Ingwe walifurika kwa wingi.

Gor Mahia ambao wanachuana na timu ya Tusker FC kwenye msimamo wa Ligi hiyo wameweza kujitengenezea nafasi ya kuikabili Tusker kwenye kombe la ligi Kuu, walianza mechi kwa matumaini ya kufanya vizuri ili kuzidi kujitengenezea matumaini ya kupunguza gepu la pointi bana yao na Tusker ,huku AFC Leopard nao wakibaini kwamba walihitaji tatu ili kuweza kupanda na kuorodheshwa katika nafasi nane bora.
Mabao ya Gor Mahia yalifungwa na Meddie Kagere na Enock Angwnda. Katika Mechi nyengine Tusker walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Nairobi City Star. Western Stima nae alitoa sare ya 1-1 na Ulinzi Stars.

No comments:

Post a Comment