![]() |
| Kalimangonga''Kally''Ongara kocha wa Majimaji. |
Baada ya kuwa na mwanzo mbaya wa msimu timu ya Majimaji ya Songea imempa ahueni kocha wake Kally Ongara baada ya kuibuka na ushindi mabao 2-1 dhidi ya Toto Africans ya mjini Mwanza.
Mchezo huo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza umeweza kuwapa ahueni ya matumaini timu hiyo ambayo iko kwenye hatua mbaya kimsimamo kwenye ligi.
Mabao ya Majimaji katika mechi hiyo yalifungwa na Peter Mapunda
katika dakika ya 30 na 80 huku bao la Toto likifungwa na Reliant Lusajo
katika dakika ya 11.
"Mchezo umeisha nadhani pointi tatu ndio muhimu kwetu tulipoanza ligi
tulikuwa tumecheza sana chini ya kiwango, lakini tumeweza kufanya
mabadiliko tukasisitiza vijana wawe wapambanaji, tulipata mwanzo mgumu
kutokana na tumeingia kambini wiki moja kabla ya Ligi Kuu kuanza lakini
sasa tunabadilika siku hadi siku,” alisema Kocha Kally.
Alisema amefurahishwa na vijana wake kwa kutengeneza nafasi nyingi
katika mechi hiyo ambapo mashuti yao mengine yalikuwa yakigonga mwamba.
"Tulikuwa nyuma ya goli moja tumepambana na kuweza kusawazisha kisha
kushinda mechi yetu. Nawaonya wachezaji wangu hakuna mtu mwenye namba
yake na pia bado tuna kazi kubwa sana ya kupambana na kushinda dhidi ya
African Lyon,” alisema.
Kocha wa Toto, Khalfan Ngassa aliwalaumu wachezaji wake na kusema
hawajitambui na wanashindwa kucheza mpira na kuwakilisha mkoa wao.
Ngassa mpaka sasa ameiongoza Toto katika mechi tatu na kupoteza mbili
dhidi ya Majimaji na Mbao FC huku akishinda moja dhidi ya Kagera Sugar.

No comments:
Post a Comment