![]() |
Kevin Durant akiwa kwenye moja ya majukumu. |
Baada ya kuwa na msimu wa mafanikio na rekodi nzuri waliyojiwekea msimu uliopita kwenye ubingwa 2015-2016, lakini walishindwa kwenye fainali dhidi ya LeBron James na Cleveland Cavaliers.
Na sasa Durant ambaye ni mchezaji wa Warriors ameweka wazi sababu iliyomfanya aweze kujiunga na timu hiyo, wakati huo akiwa Oklahoma City akitazama michezo saba ya kuamua nani awe bingwa.
Durant alisema, ''wakala wangu Rich Kleiman, alikuwepo hapa, tukitazama michezo saba.''' Kwa kweli ilianza kufunua shauku yangu, hakukuwa na maswali, hakukuwa na njia ya kwenda kwenye timu hii, nilipenda kucheza na hawa watu. Ninaweza kukimbia juu na chini kwenye uwanja, nikamuomba wakala wangu unajua nilikuwa kama vile wewe, hii inaweza kuwa nzuri kwangu.''
Huku akisema kuanguka kwa Warriors kulimsaidia yeye kufanya maamuzi ya kujiunga nayo.
''Walipoteza, na kuwa zaidi ya ukweli kila siku,'' Durant alisema. Unaanza kuanza kufikiri juu ya hilo na zaidi unanza kuangalia utakapoendana napo.
''Kisha mara moja nikakaa na hawa watu, kila kitu nilichoitaji kujua kuhusu wao, walinionyesha. Lakini hatuitaji kuzungumzia kama ingetokea Warriors wangeshinda taji, kwasababu nisingeapata kazi na wasingekuja kwangu.
''Unaweza kusema kwamba nina furaha walivyopoteza.''
No comments:
Post a Comment