Joe Hart na Wayne Rooney. |
Golkipa wa Uingereza Joe Hart amemsifia Wayne Rooney kama kiongozi wa timu ingawa nahodha huyo alitemwa dhidi ya Slovenia.
Rooney mwenye umri wa miaka 30, aliwekwa benchi kwenye mchezo huo ambao vijana wa Gareth Southgate walipata sare ya 0-0 kwenye kufuzu Kombe la Dunia Jumanne hii.
Huku Jordan Henderson akipewa majukumu ya Rooney kama nahodha wa "Three Lions", lakini Hart hakuacha kumsifia nyota huyo wa Manchester United.
Hart alisema ''kila mtu anajua kwamba Wayne ni kiongozi wetu, kila siku haijalishi anachofanya, anatuongoza,'' aliiambia Sky Sport.
''Jordan alifanya vizuri usiku wa leo, akichukua majukumu ya unahodha na kufanya Rooney kutoweza kucheza.
''Wayne alimsaidia, tulimsaidia Jordan. na tunaendelea mbelel kama timu. Na siku zote tutaendelea kufanya hivyo.
''Kuna watu wengi kwenye kikosi ambao wanahitaji kucheza na kocha anachagua na tunamuunga mkono kwa hilo.''
Pamoja na sare hiyo England bado wanaongoza kundi F wakiwa na pointi saba kutoka kwenye mechi zao tatu walizocheza.
No comments:
Post a Comment