Friday, October 14, 2016

MANCINI AMSHAURI BALLOTELI KUTOVUA JEZI AKISHANGILIA BAO LAKE.

Mario Balloteli.
Huku akiwa ana furahia kuanza vyema kwenye timu ya Nice nchini Ufaransa. Mchezaji huyo mwenye miaka 26 tayali ameshafunga mabao 5 katika mechi 3kwa klabu hiyo ya  Cote'd Azur.
Akionyesha uwezo na ahadi zake kwa klabu hiyo kwamba ilikuwa inahitaji huduma yake kwa kiwango anachoonyesha ,nakuwa furaha kati ya ndoa yake na klabu hiyo. 

''Anahitaji kufunga angalau mabao 20 msimu huu,'' meneja wa zamani wa Balloteli, Robert Mancini alisema kwenye mahojiano yake na L'Equipe kupitia Fooball Italia. Kufunga mabao mengi kutampa sifa na atajivunia hilo lakini Mancini akaongelea jambo moja na kumshauri Mario juu ya aina yake ya ushangiliaji wa kuvua jezi yake pindi anapofunga bao. 

Mancini alisema ''Mario anapaswa kuacha kuvua jezi yake mara moja anapofunga bao.'' Ili kuepuka kadi za njano kwa kuvua jezi uwanjani ingawa Mario anafanya lolote akiwa na furaha.

''Inatakiwa kuwa hali ya kawaida akifunga bao.'' 


No comments:

Post a Comment