Mreno Cristiano Ronaldo ameelezea kwamba ni ndoto yake kuendelea kubaki Real Madrid kwa miaka mingi zaidi ijayo.
Ronaldo ambaye alishinda taji la Klabu ya Mabingwa mara 3 katika maisha yake mwezi May, kabla ya kushinda la Euro akiwa na Ureno nchini Ufaransa.
Mchezaji huyo mwenye miaka 31 ana mkataba unaomuweka Santiago Bernabeu mpaka 2018 ingawa kuna taarifa inayosema atapewa mkataba wa muda mrefu.
Akizungumza wakati ambao akipokea tuzo ya Klabu ya Bingwa namba 1, ambayo upigiwa kura na wasomaji wa Marca na La Gazzetta delo Sport, Ronaldo aliweka wazi kwamba ataendelea na kazi yake akiwa Madrid.
''Nimeshinda ligi ya Klabu ya Mabingwa na Euro, ni wakati mzuri katika kazi yangu na maisha yangu ya soka,'' alisema.
''Inanifanya niongeze bidii ya kufanya kazi kwa bidii kwenye hii klabu.
''Ni ndoto yangu kuendelea kuichezea Real Madrid na kiukweli ninahitaji kuendelea kuwa hapa kwa miaka mingi zaidi sababu ni klabu yenye nafasi ya pekee moyoni mwangu.''
Ronaldo ambaye mpaka sasa ameshafunga mabao matatu kwenye mechi sita kwenye mashindano yote kwa Madrid msimu huu.

No comments:
Post a Comment