
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea barua kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Ethiopia (EFF), ikielezea juu ya kufutwa kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliokuwa ufanyike Oktoba 8, 2016.
EFF imesema kwamba imelazimika kufuta mchezo huo ulikuwa kwenye kalenda ya FIFA kwa sababu za hali ya hewa si rafiki kwa sasa nchini Ethiopia.
Mkwasa atalazimika kuvunja kambi ya timu hiyo ambayo iliwekwa katika hoteli ya Blue Pear iliyoko Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo uliratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. EFF, ndio walioomba nafasi hiyo.
Ingekuwa ni faida kwa Tanzania kama ingeshinda mchezo huo kwa maana kina alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.
No comments:
Post a Comment