Mwenyekiti wa Chama cha riadha Zanzibar akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Chama cha
riadha Zanzibar Abdulhakim Cosmas akitoa maelekezo juu ya mbio za
Kilomita 10 zilizoandaliwa na Kikosi cha KMKM katika Mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Kikosi hicho Kibweni.
Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef
Mwenyekiti wa Chama cha
riadha Zanzibar Abdulhakim Cosmas akitoa maelekezo juu ya mbio za
Kilomita 10 zilizoandaliwa na Kikosi cha KMKM katika Mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Kikosi hicho Kibweni.
Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef |
Kikosi maalum cha kuzuia magendo (KMKM) kimeandaa mashindano ya riadha ya mita 10 yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Mashindano hayo ambayo yatajumuisha wadau mbali mbali wa michezo yana lengo la kujenga mahusiano ya karibu kati ya KMKM na jamii katika kuleta maendeleo, amani, upendo na kuinua vipaji vya wanamichezo wao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Michezo wa Kikosi hicho Kapteni Khatibu Khamis Mwadini alisema kwamba mashindano hayo ni mwendelezo wa yale yaliyofanyika 2014.
Alisema, mbio hizo zitaanzia makao makuu ya kikosi chao hicho yaliyopo Kibweni na kuishia katika viwanja vya Maisara kwa kupitia maeneo ya Kinazini, Malindi, Darajani, Mkunazini, Michenzani, Kariakoo, Mafunzo na Kilimani.
Alisema katika mashindano hayo kutakuwa na kundi la wazee na watu wenye ulemavu ambao watakimbia masafa ya kilomita mbili kutoka mzunguko wa Michenzani, Madema, CCM Maisara na viwanja vya Maisara. “Katika mbio hizo pia tunategemea vikundi vya mazoezi (Kitambi Noma) visivyopungua 20 vitashiriki katika mbio hizo”, alisema.
Aidha alisema kwamba katika mashindano hayo wanatarajia kuwashirikisha na wanariadha wakongwe kama Juma Ikangaa na wengine ambao bado wanaendelea kufanya nao mazungumzo.
No comments:
Post a Comment