Friday, October 21, 2016

KAZAULA NA PIALALI KUKUTANA NOVEMBA 12.


MABONDIA Pius Kazaula wa Morogoro na Idd Pialali wa Bagamoyo Pwani, wamesaini mkataba wa kupigana Novemba 12 mwaka huu katika ukumbi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo TASUBA.


Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST), Anthony Rutagamba alisema mabondia hao watapigana kuwania mkanda wa Shirikisho la Ngumi Afrika ambalo litakuwa na raundi 12.
“Tumeamua kuwawekea ubingwa wa Afrika kwa kuwa mabondia hawa viwango vyao vinafanana katika ubora wote wana pointi tano na nyota moja hivyo ni mabondia wa kuwaendeleza kwa kuwa ndio vijana tunaowategemea kwa kipindi hiki,” alisema Rutagamba.
Rutagamba alisema mabondia hao watacheza katika uzito wa kilogramu 66 na UBO Afrika ndio watasimamia ambao mwakilishi wao atakuwa Josmo Mlundwa.
Mabondia wengine walioingia mikataba kwa ajili ya kucheza mchezo wa utangulizi siku hiyo ni Emilio Norfat atakayepigana na Rojas Masamu pambano la raundi sita katika uzito wa kilogramu 61.

No comments:

Post a Comment