![]() |
| Hugo Lloris, Tottenham. |
Sahau kuhusu Petr Cech, David De Gea na Thibaut Courtois, Hugo Lloris ni kipa bora kwenye Premier League, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa tottenham Eric Dier. Kipa huyo ambaye ni nahodha wa Tottenham, toka msimu uliopita amekuwa kwenye kiwango kizuri cha majukumu yake akiwa golini. Sare dhid yao na Bournemouth Jumamosi iliyopita imemfanya azidi kujiongezea uwezo wa kazi bora kwa msimu huu wa 2016/2017.
Dier amemsifu raia huyo wa Ufaransa kwa kusema ''kwangu ni kipa bora na kipa bora kwenye ligi.''
Tottenham ni timu pekee kwenye Premier League ambayo haijafungwa mpaka sasa, huku kipa huyo akiruhusu mabao manne katika mechi tisa bila kusahau changamoto waliyoipata baada ya kupoteza kwa Leicester City mwezi May.
![]() |
| Lloris na Dier kwenye majukumu yao ya timu ya taifa ya Ufaransa na England. |
''Anadharauliwa. Sijui kwanini inakuwa hivyo, pengine ni kwa sababu ya hali yake ya chini. Ni mzuri kimawazo. Anavutiwa na kucheza soka pekee.
''Siyo tu kwasasa. Msimu uliopita amefanya vizuri katika kuokoa pia. Na sasa tunaona pia kwenye msimu huu.
''Anafanya kila kitu. Pale unapocheza dhidi ya mshambuliaji wa haraka, kama Bournemouth walivyokuwa nao, sio kwamba ni mzuri kwenye eneo lake, lakini pia ni kipa anaetoka kwenye eneo lake.
''Sidhani kama kuna mwingine mzuri kama yeye, kusema ukweli, lakini hayo ni mawazo yangu na soka ni mchezo wa mawazo.''


No comments:
Post a Comment