Kuelekea mechi yao ya marudiano dhidi ya Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa, kocha Pep Guardiola amesisitiza kwamba mipango yake mikubwa zaidi iko kwa timu yake na sio wageni wao. Manchester City ambao walipoteza kwenye mchezo wao wa kwanza kwenye uwanja wa Nou Camp walilala 4-0 huku nyota Lionel Messi akifunga hat-trick kwenye ushindi hu, huku Pep akisisitiza kujiamini zaidi baada ya ushindi 4-0 waliopata dhidi ya West Brom Jumamosi iliyopita.
''Kushinda mechi iliyopita kumetusaidia sana,'' aliongeza Pep.
Pep aliongeza kuwa ''kujiamini kwetu kumeongezeka sana, lakini Ligi ya Mabingwa ni ushindani tofauti, ni mfupi sana na sisi tuna haja ya kufanya hivyo dhidi ya timu bora.
Akizungumzia namna ya mabao yalivuofungwa kwenye mchezo wa awali amesema kwamba baadhi ya wachezaji wake wanabidi wawe makini.
''Tulifungwa 4-0 hivyo tuna mengi ya kujifunza, alisema.
''Baadhi ya wachezaji wetu, ilikuwa mara yao ya kwanza Nou Camp, lakini walicheza vizuri.
Kocha huyo wa zamani wa Bayern Munich ameshuhudia wachezaji wake watano wakikaa nje katika mechi zao tano kuelekea mchezo huo alisema kwamba ''ni vigumu kuwafunga ukiwa 11 na ngumu zaidi ukiwa 10,'' aliongezea.
Will Caballero amechukua nafasi ya Claudio Bravo ambaye ana kadi nyekundu aliyopata kwenye mchezo uliopita.
No comments:
Post a Comment