Sunday, October 30, 2016

YANGA DIMBANI LEO UHURU, MNYAMA ANA SPIDI YA 4G.


Ligi Kuu ya Vodacom  inaendelea leo kwa timu ya Yanga kuikaribisha Mbao FC kwenye uwanja wa Uhuru, Yanga ambayo itakuwa chini ya kocha wake Hans van Pluijm alierudi kuifundsha timu hiyo baada ya kujiuzulu nafasi ya ukocha baada ya uongozi wa klabu ya wanajangwani kumleta kocha mpya huku wakiwa na mkataba na Mholanzi huyo kitendo alichokiona amedharauliwa.

Na hapo jana kwenye Uwanja wa Kambarage Simba imeendeleza wimbi lake la kutopoteza mechi mfululizo kwa msimu huu baada ya kuifunga Mwadui ya Shinyanga bao 3-0 mabao ya Simba yalifungwa na Mo Ibrahim dakika ya 23 Mo na dakika ya 45 Kichuya akafunga bao la pili kabla ya Mo Ibrahim tena kufunga bao la tatu kwa Simba dakika ya 50 na kufanya matokeo hayo kwa Simba kuendelea kukaa kileleni  mwa Ligi.

Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Bara, Toto Africans ya Mwanza jana iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Mabao ya Toto yalifungwa na Waziri Junior, Hamim Abdul, Omege Seme huku yale ya Mtibwa Sugar yalipachikwa na Kelvin Friday.

Kutoka Mbeya, timu ya Mbeya City imefanya kweli baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Majimaji ya Songea katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Katika mechi zingine; JKT Ruvu iliutumia vizuri uwanja wao baada ya kuifunga Ndanda FC kwa bao 1-0 huku bao hilo pekee likifungwa na Atupele Green, na African Lyon ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Prisons.

No comments:

Post a Comment