Sunday, October 16, 2016

MANCHESTER UNITED WAMPA MKATABA JOHNSTONE.

Sam Johnstone.

Golikipa Sam Jphnstone ameweza kusaini mkataba mpya na ''red devils'' mkataba utakao muweka Old Traford mpaka 2018, huku kukiwa na makubaliano ya kuongeza mkatba zaidi kwa miaka mingine ijayo.
Kipa huyi mwenye umri wa miaka 23 amekuwa klabuni hapo kwa zaidi ya miaka 13, na bado hajaanza kuonekana kwenye Premier League akiwa na United.

Lakini kocha wa United Jose Mourinho anaamini Johnstone ana maendeleo ya haraka na atakaekuwa na nafasi klabuni hapo kwa siku za usoni. 

Mourinho alisema ''Sam ni golikipa mwenye uwezo mzuri,''. Ni mtaalamu ambaye bado ni mdogo  mwenye ushawishi kwenye michezo.   

''Ana maendelelo mazuri kiasi cha muda mfupi nilichokuwepo klabuni hapa nimeliona hilo nina imani anajitengenezea mustakabali wake akiwa United.'' 

Johnstone ambaye amewahi kutolewa kwa mkopo kwenye klabu nyingi kama Walsall, Doncaster Rovers na Prestone North End, anazani akifanya mazoezi na David De Gea na Sergio Romero kutamuongezea kiwango na ujuzi.    

''Nina furaha kusaini mkataba mpya,'' alisema Johnstone. Niko kwenye klabu toka nikiwa na maika 10 na nimeweza kukua hapa.  

''Miaka 13 imepita na nina furahia kila hatuia ya maisha nyangu hapa.     

''Nina fanya kazi na magolikipa wa kisasa duniani kila siku na sasa ninakwenda kutumua ujuzi wangu na kumshawishi kocha ninachoweza kufanya.

No comments:

Post a Comment